Header Ads

Rais Trump Asema Ataunga Mkono Mipango Yote Ya Kutimiza Amani Kati Ya Israel Na Palestina

Tokeo la picha la trmp Donald

Rais Donald Trump wa Marekani amesema ataunga mkono mpango wa "nchi moja" au "nchi mbili" katika kutimiza amani ya Israel na Palestina. Kauli hiyo ni tofauti na msimamo wa serikali za zamani za Marekani wa kuunga mkono mpango wa "nchi mbili".

Kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kukutana na Waziri mkuu wa Israel Bw Benjamin Netanyahu, Bw Trump amesema anaweza kukubali mpango wowote unaokubaliwa na Israel na Palestina, na Marekani itaendelea na juhudi za kuhimiza nchi hizo mbili kufikia makubaliano ya amani, lakini ni lazima pande hizo mbili zifanye mazungumzo ya moja kwa moja.

Kauli hiyo imelaaniwa na watu wa Palestina kwa kuwa imeonyesha upendeleo wa wazi kwa upande wa Israel. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres amesema hakuna mpango mbadala wa ufumbuzi wa nchi mbili kwa mgogoro wa Mashariki ya Kati.

No comments

Powered by Blogger.