Header Ads

Rais Mugabe Aonya Wanachama Kutofanya Hila Kutafuta Uongozi

Tokeo la picha la President Mugabe

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewaonya wanachama dhidi ya vitendo vya kufanya hila kutafuta nyadhifa za uongozi, huku mvutano kuhusu mrithi wa nafasi yake ukizidi kupamba moto katika chama chake cha Zanu-PF.

Rais Mugabe amesema badala ya kufanya hila, viongozi hodari wanachaguliwa na umma kwenye msingi wa sifa zao na uchapa kazi.

Rais Mugabe alisema hayo katika sherehe ya miaka 93 ya kuzaliwa iliyoandaliwa na ofisi yake, hata hivyo alikanusha kuhusu uwepo wa makundi katika chama chake yanayosubiri kumrithi.

Hivi karibuni rais Mugabe amesema hajajiandaa kuondoka madarakani na pia hatatafuta mrithi wake, kwa sababu huu ni wajibu wa wananchi.

No comments

Powered by Blogger.