Header Ads

Radamel Falcao: Man Utd, Chelsea Zilitaka Kuniia Kisoka

Tokeo la picha la Radamel Falcao 2017

Mshambuliaji wa AS Monaco Radamel Falcao amezituhumu klabu za Man Utd na Chelsea kwa kusema zilikaribia kuua soka lake.

Falcao amefunguka suala hilo, alipozungumzia safari yake ya kwanza ya England baada ya kuondoka mwishoni mwa msimu uliopoku Chelsea.

Kesho klabu ya AS Monaco inayotumikiwa na Falcao, itapambana na Man City katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa 16 bora wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwenye uwanja wa Etihad.

Falcao amesema ilikua vigumu kuonyesha uwezo wake wakati akiwa na klabu ya Man Utd na Chelsea kutokana na nafasi finyu ya kucheza mara kwa mara aliyoipata.

Amesema wakati mwingine alitamani kuacha soka kabisa kutokana na changamoto alizozipitia akiwa nchini England, lakini kuvumilia na kuamini bado alikua na uwezo wa kucheza soka vilimsaidia hadi ilipofikia wakati wa kurejea As Mocano.

"Nilipitia wakati mgumu sana, lakini sina budi kuamini ilikua ni sehemu ya mapito ya soka langu ".


"Ninaweza kusema nilipoteza wakati mwingi wa kujiendeleza katika soka la ushindani." Alisema Falcao. 

No comments

Powered by Blogger.