Header Ads

PSG Yaisasambua FC Barcelona

Tokeo la picha la psg 4-0 Barcelona
Mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain wamewasasambua mabingwa wenzao kutoka Hispania FC Barcelona, kwa kuwashindilia mabaoa manne kwa sifuri katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Mchezo huo uliounguruma kwenye uwanja wa Parc des Princes jijini Paris ulishuhudia mabao ya mabingwa wa Ufaransa yakipachikwa wavuni na Angel Di Maria aliyefunga mabao mawili, Julian Draxler na Edinson Cavani.
Ushindi huo kwa PSG ni hazina nzuri kwao kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili ambao utachezwa majuma mawili yajayo mjini Barcelona nchini Hispania.
Endapo FC Barcelona watahitaji kusonga mbele kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu, watalazimika kupata ushindi wa mabao matano kwa sifuri ama zaidi.
Hii inakua ni mara ya kwanza kwa PSG kuwabanjua Barcelona kwa kuwachapa kipigo cha mbwa mwizi katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Kwa mara ya mwisho wawili hao walipokutana kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya FC Barcelona walichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri msimu wa 2014/15.

No comments

Powered by Blogger.