Header Ads

Pep Guardiola Asikitishwa Na Kampeni Za Kumng'oa Wenger

Tokeo la picha la Pep Guardiola and Wenger

Meneja wa Man City Pep Guardiola amepingana na vyombo vya habari, namna vinavyoripoti taarifa zinazomuhusu bosi wa kikosi cha Arsenal Arsene Wenger.

Pep Guardiola ameonyesha kuchukizwa na kitendo cha vyombo vya habari kumuandama meneja huyo kutoka nchini Ufaransa, kufuatia sakata la kushinikizwa aondoke mwishoni mwa msimu huu pindi mkataba wake utakapofikia kikomo.

Guardiola alizungumza mwishoni mwa juma lililopita na baadhi ya vyombo vya habari kwa kusema, hatua zinazochukuliwa dhidi ya mzee huo “HAZIKUBALIKI” kutokana na kwenda kinyume na utaratibu.

Alisema inasikitisha kuona vyombo vya habari vikiwa sehemu ya kushinikiza mzee huyo kuondoka, na hajui kwa nini inafikia hatua hiyo, wakati chombo cha habari kinapaswa kuwa katikati kwa kutangaza habari za usawa.

"Nimesikia mengi kuhusu Wenger, lakini sikubaliani na utaratibu unaochukuliwa na vyombo vya habari, hata kama wanatumia namna ya kuwahoji wachezaji wa zamani, bado ninaamini sio sawa.”


"Kazi yetu inahitaji uvumilivu, na hata ikitokea unatakiwa kuondoka taratibu zinachukuliwa kiungwana na sio kumshupalia mtu kwa kumpigia kelele ambazo hazina mantiki yoyote.” Alisema Guardiola.

No comments

Powered by Blogger.