Header Ads

Paulo Dybala Kubaki Juventus FC

Tokeo la picha la Paulo Dybala

Ndoto za Real Madrid za kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Argentina na klabu ya Juventus Paulo Dybala, zimeanza kufifia kufuatia mazungumzo ya kusainiwa kwa mkataba mpya huko mjini Turin kwenda kama yalivyotarajiwa.

Dybala huenda akasaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa soka nchini Italia mwezi huu, baada ya kuhakikishia mahitaji yake yataingizwa katika mkataba huo.

"Tumefikia pazuri na ninaamini wakati wowote kuanzia sasa nitasaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Juventus FC," Dybala aliiambia Sky Italia.

“Kuna baadhi ya vitu vilikua havijakaa sawa, ndio maana mambo yamechelewa, lakini kwa sasa ninaweza kusema kila kitu kipo vizuri.


"Wakala wangu alikua Italia kushiriki sehemu ya mazungumzo ya kusainiwa kwa mkataba mpya, na ninashukuru amesaidia mambo mengi kwa kumtaka rais Giuseppe Marotta kuweka mambo ya msingi niliyokua nayahitaji, ili niweze kufanikisha azma hii.'

No comments

Powered by Blogger.