Header Ads

Pande Zinazozozana Ukraine Zafikia Makubaliano Kuhusu Kuondoa Silaha Nzito

Tokeo la picha la OSCE and Russia

Kundi la kushughulikia mgogoro wa Ukraine linaloshirikisha Ukraine, Shirika la Ushirikiano na Usalama la Ulaya OSCE na Russia, lilikutana mjini Minsk, ambako pande zinazozana huko Ukraine zimefikia makubaliano kuhusu kuondoa silaha nzito kutoka maeneo yenye mapigano kabla ya tarehe 20 Februari.

Mjumbe maalumu wa Shirika la Ushirikiano na Usalama wa Ulaya amewaambia waandishi wa habari kuwa masuala ya kusitisha vita na kuweka eneo salama kwa ajili ya kuwalinda raia na miundombinu ya kiraia yalizungumzwa kwenye mkutano. 

Pia amesema tangu kundi hilo likutane tarehe mosi mwezi huu, operesheni za kijeshi mashariki mwa Ukraine zimepungua kidhahiri.

No comments

Powered by Blogger.