Header Ads

Nigeria Yaitaka Afrika Kusini Kuwalinda Raia Wake Katika Mashambulizi Dhidi Ya Wageni

Tokeo la picha la Abike Dabiri-Erewa

Nigeria imeitaka serikali ya Afrika Kusini ichukue hatua madhubuti kuwalinda raia wa Nigeria na watu kutoka nchi nyingine za Afrika wanaoishi nchini humo katika mashambulizi yanayotokana na chuki dhidi ya wageni.

Msaidizi mwandamizi wa rais anayeshughulikia mambo ya nje na uhamiaji Bibi Abike Dabiri-Erewa ameyataja mashambulizi hayo kuwa ni kitendo cha kurudi nyuma kisicho cha lazima.

Bibi Dabiri-Erewa ameutaka Umoja wa Afrika kuingilia kati haraka mashambulizi yanayotokea dhidi ya wanigeria na waafrika wengine wanaoishi nchini humo.

Habari nyingine zinasema, kamati ya bunge la Afrika Kusini inayoshughulikia mambo ya polisi imesema, mashambulizi dhidi ya wageni yaliyotokea huko Rosettenville na magharibi mwa Pretoria yangeweza kuzuilika kama polisi wangechukua hatua kwa wakati.

Imefahamika kuwa nyumba 15 za wanigeria zilichomwa moto wiki iliyopita kwenye maeneo hayo, na watuhumiwa sita wamekamatwa na polisi.

No comments

Powered by Blogger.