Header Ads

Nigeria Kucheza Dhidi Ya Senegal, Burkina Faso

Tokeo la picha la The Super Eagles Vs Tanzania

Shirikisho la soka nchini Nigeria limethibitisha uwepo wa michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki, ambayo itashuhudia timu ya taifa ya nchi hiyo ikipambana na Senegal (Simba Wa Teranga) pamoja na Burkina Faso (The Stalion).

michezo hiyo itatumika kama sehemu ya kukiandaa kikosi cha Nigeria kwa ajili ya michezo ya kuwania kufuzu fainali za Afrika za mwaka 2019 pamoja na zile za kombe la dunia za mwaka 2018.

Nigeria itaanza kucheza dhidi ya Senegal Machi 23 mjini London na siku nne baadae itapapatuana na Burkina Faso.

Senegal watacheza mchezo huo ambao utakua wa kwanza kwao, tangu waliposhindwa kufurukuta katika mtanange wa robo fainali wa fainali za Afrika zilizofanyika nchini Gabon kwa kufungwa na Cameroon, hali kadhalika kwa Burkina Faso watakua wakicheza mchezo wao wa kwanza tangu walipomaliza katika nafasi ya tatu kwenye fainali hizo.


Katika harakati za kuwania nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2018, Nigeria inaongoza kundi B kwa kuwa na point 6 zilizopatikana baada ya ushindi wa michezo miwili, na kwa upande wa kuwania nafasi ya kucheza AFCON ya 2019 timu hiyo imepangwa na Afrika kuisni, Libya na Shelisheli.

No comments

Powered by Blogger.