Header Ads

Nchi Za Afrika Zatakiwa Kuongeza Nguvu Kwenye Uvumbuzi Ili Kukwepa Mitikisiko Ya Kiuchumi


Nchi za Afika kusini mwa Sahara zimetakiwa kukumbatia sera ya uvumbuzi ili kuimarisha unyumbufu wa uchumi wao kutokana na mitikisiko ya nje ikiwemo kushuka kwa ukuaji wa uchumi wa dunia na mwenendo usitabirika wa hali ya hewa.


Akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano la ngazi ya juu la uvumbuzi uliofanyika jijini Nairobi nchini Kenya, waziri wa biashara na masuala ya Afrika Mashariki wa Kenya Phyllis Kandia amesema, nchi za Afrika zina uwezo wa kukabiliana na mitikisiko inayohusiana na kushuka kwa bei ya bidhaa na wimbi la kupinga utandawazi kutoka magharibi, endapo serikali zitatoa kipaumbele kwenye sera ya mageuzi, biashara ya kuvuka mpaka, na kuchochea uvumbuzi kwa vijana.

No comments

Powered by Blogger.