Header Ads

Tokeo la picha la oliver Khan 2017

Mlinda mlango anaeendelea kukumbukwa duniani kote Oliver Rolf Kahn, ameonyesha kuguswa na kipigo cha mabao matano kwa moja walichokapata Arsenal kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa 16 bora wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya FC Bayern Munich.

Khan ambaye alitamba akiwa na timu ya taifa ya Ujerumani kuanzia mwaka 1995 hadi 2006 amesema ilimsikitisha kuona hali hiyo ikitokea mjini Munich usiku wa kuamkia jana, lakini amebaini jambo kubwa ambalo linakitafuna kikosi cha Arsenal.

Khan ambaye pia aliitumikia FC Bayern Munich kwa mafanikio makubwa kuanzia mwaka 1994 hadi 2008, amesema kuna hali ya sintofahamu inayoendelea kati ya wachezaji wa The Gunners dhidi ya meneja wao Arsene Wenger.

Amedai baadhi ya wachezaji hawana imani ya kutosha dhidi ya meneja huyo ambaye anapigiwa kelele na mashabiki kwa kutakiwa aondoke baada ya kukaa muda mrefu bila mafanikio ya kutwaa mataji makubwa kama ligi ya England na ligi ya mabingwa barani Ulaya.

"Kuna baadhi ya wachezaji wanamchukulia poa meneja wao, hawamuamini kwa asilimia zote," Alisema Kahn.


Khan amesisitiza kuwa, katika klabu yoyote pakitokea hali ya kutoamini ni lazima majanga yatajitokeza, hivyo kuna ulazima wa suala hilo ikaondolewa kwa kufanyika maamuzi magumu.

No comments

Powered by Blogger.