Header Ads

Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Amuagiza Dc Makete Kuunda Tume


Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka(wapili kushoto) akiangalia athari za moto wa bweni hilo.

Mabaki ya vitu vya wanafunzi vilivyoteketea kwa moto katika bweni hilo.

Mkuu wa mkoa akizungumza na wanafunzi shuleni hapo.


Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy ameagizwa kuunda tume ya kuchunguza tukio la kuwaka moto bweni la wasichana liitwalo Serengeti La Itamba sekondari pamoja na bweni lingine la wasichana lililoungua jumamosi iliyopita

Agizo hilo limetolewa Jana na Mkuu wa mkoa wa Njombe Mh. Christopher Olesendeka alipotembelea shule hiyo kujionea athari za moto huo ulioteketeza bweni moja lote 

Amesema serikali haiwezi kukubali na ni lazima chanzo cha moto huo kijulikane na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wahusika endapo uchunguzi utabainisha kuwa kuna watu wamehusika

Mh Olesendeka amesema serikali haiwezi kukubali vitendo vya moto kuendelea kuunguza shule mbali mbali hapa nchini 

Pia ameuagiza uongozi wa shule hiyo kuweka Mazingira mazuri kubaini ukweli wa hujuma kama hizi zinazoweza kujitokeza lakini pia kama kuna dosari mbali mbali miongoni mwa wanafunzi au shule nzima zijulikane ili ufumbuzi upatikane 


No comments

Powered by Blogger.