Header Ads

Mjumbe Maalum Wa Rais Xi Jinping Wa China Ahudhuria Sherehe Ya Kuapishwa Kwa Rais Adama Barrow Wa Gambia

Mjumbe maalum wa rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa mkutano wa halmashauri ya kisiasa wa China Ma Peihua tarehe 18 mwezi Februari alihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais Adama Barrow wa Gambia iliyofanyika Banjul nchini Gambia. Kabla ya sherehe hiyo, rais Barrow alikutana na Ma Peihua.

Ma Peihua alitoa pongezi ya dhati na matumaini mazuri ya rais Xi Jinping kwa rais Barrow akieleza kuwa, tangu kurudishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Gambia mwezi Machi mwaka jana, nchi hizo mbili zimerudisha ushirikiano katika sekta za siasa, uchumi na biashara, utamaduni wa binadamu. 

Kurudishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kwa nchi hizo mbili kunalingana na maslahi ya muda mrefu na msingi ya watu wa nchi hizo mbili.

Rais Barrow alimshukuru rais Xi Jinping kwa kutuma mjumbe maalum kuhudhuria sherehe yake ya kuapishwa, na kumtaka Bw. Ma Peihua amsalimie rais Xi Jinping kwa niaba yake.

No comments

Powered by Blogger.