Header Ads

Mb Dogg: Muziki Ni Kupanda Na Kushuka

Tokeo la picha la mb dogg

Msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyefanya vizuri sana miaka ya nyuma kwa nyimbo nzuri zenye mpangilio wa sauti zenye mvuto Mbwana Mohamed, anayejulikana kwa jina la 'Mb Dogg', ameeleza kuhusiana na uelekeo wake wa muziki.

Mb Dogg ameeleza muziki ni kama upepo, ambapo kwa kipindi hiki unaonekana upepo haupo kwake kutokana na kimya kingi kilichomtawala juu ya muziki wake kiasi ambacho ni athari kwake kwani kupitia ukimya huo anapoteza mashabiki wengi walio mwamini na kuukubali muziki wake.

Akizungumza Dar es salaam jana, Mb Dogg amesema anaomba mashabiki wake wamuelewe ila ipo siku upepo utakubali uelekeo wake na atarejesha makali yake ya zamani.

Pia alieleza muziki ni kama maisha kuna kupanda na kushuka, aliendelea kwa kusema kuna mipango ambayo anaipanga kwa sasa na uongozi wake na mambo yatakaa sawa atarudi kwenye  fani kwakuwa sasa kuna simu nyingi zinamuhamasisha kurudi kwenye muziki.

No comments

Powered by Blogger.