Header Ads

Mawaziri Wakuu Wa China Na Ufaransa Wakutana Beijing

Waziri mkuu wa China Li Keqiang jana alikutana na mwenzake wa Ufaransa  Bernard Cazeneuve hapa Beijing. 

Kwenye mazungumzo yao  Li Keqiang amesema, China inapenda kuimarisha ushirikiano na Ufaransa kwenye sekta za nishati ya nyuklia, usafiri wa anga, kilimo, matibabu na uhifadhi wa mazingira. 

Cazeneuve amesema Ufaransa inapenda kushirikiana na China katika sekta mbalimbali, na pia inapenda kufanya juhudi pamoja na China kulinda uhuru wa kibiashara na kuondoa sera za kujilinda kibiashara

No comments

Powered by Blogger.