Header Ads

Mauricio Pochettino Alia Na Bahati Ya Ushindi

Meneja wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino anaamini kikosi chake kinapita kwenye wakati mgumu, kufuatia matokeo mabaya yanayomuandama kwenye michuano ya barani Ulaya.
Spurs wamepoteza mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 32 bora ya Europa League, kwa kufungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya K.A.A Gent ya nchini Ubelgiji.
Pochettino aliwaambia waandishi wa habari baada ya mchezo huo uliounguruma Ghelamco Arena, kikosi chake kimekua na bahati mbaya kwa msimu huu, kutokana na uhalisia wa mambo yanayoonekana kwenye michuano ya barani Ulaya.
Alisema hali hiyo ilianza kuonekana tangu wakiwa kwenye harakati za kutaka kusonga mbele katika michuano ya ligi ya mabingwa barani humo, lakini mambo yaliwaendela kombo na kujikuta wakitupwa hadi kwenye michuano ya Europa League.
Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini Argentina, amesisitiza kuwa na matumaini makubwa ya kukiona kikosi chake kikirejea kwenye harakati za kupambana na kuhakikisha kinapata ushindi kwenye mchezo wa mkondo wa pili ambao utachezwa juma lijalo jijini London.
Bao pekee na la ushindi la K.A.A Gent lilifungwa na Jeremy Perbet katika dakika ya 59.
Spurs watalazimika kusaka ushindi wa mabao mawili kwa sifuri ama zaidi ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano ya Europa League.
Matokeo ya michezo mingine ya hatua 32 bora ya Europa League.
FC Krasnodar 1 – 0 Fenerbahce
AZ Alkmaar 1 – 4 Olympic Lyon
Astra Giurgiu 2 – 2 Genk
Borussia Moenchengladbach 0 – 1 Fiorentina
Celta Vigo 0 – 1 Shakhtar Donetsk
C Rostov 4 – 0 Sparta Prague
Ludogorets Razgrad 1 – 2 FC Koebenhavn
Olympiacos 0 – 0 Osmanlispor FK
Anderlecht 2 – 0 Zenit St. Petersburg
Athletic Bilbao 3 – 2 APOEL Nicosia
Hapoel Beer Sheva 1 – 3 Besiktas
Legia Warszawa 0 – 0 Ajax
Manchester United 3 – 0 Saint-Etienne
PAOK Thessaloniki FC 0 – 3 Schalke 04

Villarreal 0 – 4 Roma 

No comments

Powered by Blogger.