Header Ads

Mashirika Ya Nchi Za Afrika Mashariki Yazindua Kikundi Cha Kuhimiza Malengo Ya Umoja Wa Mataifa

Tokeo la picha la Adan Mohamed - kenyaAdan Mohamed 

Mashirika ya nchi za Afrika mashariki yamezindua kikundi cha kueneza mafanikio ya malengo 17 ya maendeleo endelevu.

Waziri wa viwanda, biashara na ushirika wa Kenya  Adan Mohamed amewaambia waandishi wa habari mjini Nairobi kuwa kikundi hicho ambacho kitaundwa na watu kutoka sekta mbalimbali, kitaweka mipango kwa sekta binafsi kuisaidia serikali kutimiza malengo ya maendeleo endelevu.

Bw Mohamed amesema kikundi hicho kitayawezesha makampuni ya Afrika Mashariki kuwa na mitindo ya biashara inayohusishwa na malengo ya maendeleo endelevu kwenye mikakati yao.

Ametaja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni pamoja na utoaji wa maji, afya, elimu na huduma nyingine za kijamii.

No comments

Powered by Blogger.