Header Ads

Mashirika Ya Kibinadamu Yatafuta Dola Bilioni 1.6 Kuwasaidia Sudan Kusini

Tokeo la picha la Eugene Owusu

Mashirika ya kibinadamu yanatafuta dola bilioni 1.6 za kimarekani kwa ajili ya misaada ya kuokoa maisha na ulinzi kwa watu milioni 5.8 nchini Sudan Kusini mwaka huu.

Mratibu wa mambo ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Eugene Owusu amesema, hali ya kibinadamu nchini humo inazidi kuwa mbaya kutokana na mapambano yanayopamba moto, kudidimia kwa uchumi na mabadiliko ya hali ya hewa.

Owusu amesema mwaka huu utakuwa na mahitaji makubwa zaidi katika sehemu mbalimbali, ambapo mahitaji hayo yataongezeka katika majira yenye mavuno kidogo.

No comments

Powered by Blogger.