Header Ads

Masau Bwire: Tunakwenda Kuizika Yanga

Tokeo la picha la Masau Bwire

Hata kama mambo yao bado si mazuri sana, Ruvu Shooting wamesema wanachotaka sasa ni kuimaliza Yanga wakitoa mfano wa "kuzika"

Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kwa kuwa Yanga "walishauwawa" kwa kufungwa na Mnyama Simba mabao 2-1, wao kazi yao itakuwa ni "kuzika".

"Si unajua Yanga aliishauwawa na Simba kule poroni, sisi tunakutana nao Jumatano na kazi yetu inakuwa ni kuzika tu.


"Tutakwenda na kuwazika na kumalizia kazi. Tumejipanga na tunataka kupata pointi tatu ili turekebishe mambo yetu," alisema.

No comments

Powered by Blogger.