Header Ads

Mark Clattenburg Kuzikimbia Figisu Figisu Za England

Tokeo la picha la Mark Clattenburg

Mwamuzi Mark Clattenburg anatarajia kuondoka nchini England na kutimkia Saudi Arabia, ambapo ataendelea na shughuli zake za usimamizi wa sheria 18 za mchezo wa soka.

Bodi ya waamuzi nchini England (PGGMOL) imethibitisha kuondoka kwa mwamuzi huyo mashuhuri katika ligi ya nchini humo pamoja na barani Ulaya.

"PGMOL Inapenda kumtakia kila la kheri Mark Clattenburg katika majukumu mapya katika shughuli zake za uamuzi huko Saudi Arabia," imeeleza taarifa iliyotolewa na bodi hiyo.
"Tangu alipojiunga PGMO mwaka 2004, Mark amekua msaada mkubwa kwa waamuzi wengine kwa kutoa elimu na ushauri, ambao ulisaidia kuwajenga waamuzi wetu katika shughuli zao za kila siku.
“Tutaendelea kuumbuka na kuuthamni mchango wake alioutoa akiwa PGMOL, na bado tutaendelea kushirikiana nae kwa kumtaka ushauri ama msaada pale itakapohitajika.”
Mark Clattenburg aliweka historia ya kuwa mwamuzi pekee aliyechezesha fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu uliopita na baadae alipewa jukumu kama hilo wakati wa michuano ya Euro 2016 iliyofanyika nchini Ufaransa.

Clattenburg anakwenda Saudi Arabia, ikiwa ni baada ya mwamuzi mwingine kutoka England Howard Webb kutangaza kujiuzulu nafasi ya ukuu wa kitengo cha wamuzi nchini humo.

No comments

Powered by Blogger.