Header Ads

Marais Wa China Na Italia Wakutana Mjini Beijing

Rais Xi Jinping wa China jana hapa Beijing alikutana na mwenzake wa Italia Sergio Mattarella na kukubaliana kuendeleza uhusiano kati ya nchi zao ufikie ngazi mpya na kuwanufaisha zaidi watu wa nchi zao. 

Kwenye mazungumzo rais Xi ameikaribisha Italia kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda mmoja na Njia moja", na kujenga jukwaa kubwa zaidi la ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. 

Rais Mattarella amesema Italia inapenda kushirikiana na China kwa pande zote katika kusukuma mbele mawasiliano ya kiutamaduni kati ya nchi mbili, chini ya mfumo wa "Ukanda mmoja na Njia moja".

No comments

Powered by Blogger.