Header Ads

Man Utd Yasonga Europa League Kwa Kishindo

Manchester United's Henrikh Mkhitaryan celebrates scoring their first goal with team mates

Klabu ya Man Utd imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya Europa League baada ya kuifurusha Saint-Etienne ya Ufaransa kwa kuifunga bao moja kwa sifuri kwenye mchezo wa mkondo wa pili uliounguruma usiku wa kuamkia leo.

Bao pekee la Mashetani wekundu lilifungwa na kiungo mshambuliaji kutoka nchini Armenia Henrikh Mkhitaryan katika dakika ya 17.
Hata hivyo Man Utd walimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya beki wao kutoka Ivory Coast Eric Bailly, kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa 32 bora ya Europa League uliochezwa juma lililopita mjini Manchester, Man Utd walishinda mabao matatu kwa sifuri, hivyo wanasonga mbele kwa jumla ya mabao manne kwa sifuri.

Matokeo ya michezo mingine ya Europa League iliyochezwa usiku wa kuamkuia leo.
Fenerbahce 1 – 1 FC Krasnodar
Schalke 04 1 – 1 PAOK Thessaloniki FC.

Michuano hiyo inaendelea tena hii leo.
Osmanlispor FK Vs Olympiacos
APOEL Nicosia Vs Athletic Bilbao
Ajax Vs Legia Warszawa
Besiktas Vs Hapoel Beer Sheva
Roma Vs Villarreal
Zenit St. Petersburg Vs Anderlecht
FC Koebenhavn Vs Ludogorets Razgrad
Fiorentina Vs Borussia Moenchengladbach
Genk Vs Astra Giurgiu
Lyon Vs AZ Alkmaar
Shakhtar Donetsk Vs Celta Vigo
Sparta Prague Vs FC Rostov

Tottenham Hotspur Vs Gent 

No comments

Powered by Blogger.