Header Ads

Man City Waacha Kilio Dean Court

Manchester City's Sergio Aguero celebrates scoring their second goal

Matajiri wa mjini Manchester (Man City) wameichapa Bournemouth mabao mawili kwa sifuri katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka nchini England.

Ushindi huo umeiwezesha Man City kurejea kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo.

Kwa ushindi huo Man City wamefikisha pointi 52, ikiwa ni pointi nane nyuma ya Chelsea wanaoongoza msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 60. Hata hivyo ushindi wa Man City huenda ukawa umeingia doa, kufuatia kuumia kwa mshambuliaji kutoka nchini Brazil Gabriel Jesus.


Mabao ya Man City yalifungwa na Raheem Sterling huku Tyrone Mings akijifunga mwenyewe.

No comments

Powered by Blogger.