Header Ads

Man City: Sergio Kun Aguero Hauzwi


Matajiri wa mjini Manchester Man City, wamesisitiza suala la kutokua tayari kumuuza mshambuliaji wao kutoka nchini Argentina Sergio Kun Aguero, ambaye hakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza katika michezo miwili ya iliyopita.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alisaini mkataba mpya mwanzoni mwa msimu huu, na hatua hiyo ilimaanisha ataendelea kukaa klabuni hapo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Aguero, alitumika kama mchezaji wa akiba katika mpambano dhidi ya Swansea City, na aliingia uwanjani dakika saba kabla ya kipyenga cha mwisho akichukua nafasi ya mshambuliaji Gabriel Jesus.


Hali hiyo iliwashtua mashabiki na wadau wa soka wanaoifuatilia klabu hiyo ya Etihad Stadium, na minong’ono ya kuwa mbioni kuuzwa kwa mshambulaiji huyo iliendelea kupewa nafasi kubwa, kabla ya uongozi wa juu wa Man City kukanusha taarifa hizo.

No comments

Powered by Blogger.