Header Ads

Majeshi Ya Iraq Yazindua Operesheni Mpya Ya Kutwaa Eneo La Magharibi La Mosul

Tokeo la picha la Iraq army in mosul

Vikosi vya usalama vya Iraq vimetangaza kuanza kwa operesheni mpya ya kutwaa eneo la magharibi mwa mji wa Mosul kutoka kwa wapiganaji wa kundi la IS.

Jeshi la Iraq, polisi na baadhi ya wanamgambo wa kundi la Hashd Shaabi walianza operesheni hiyo jana kutoka kusini na magharibi mwa mji wa Mosul, na kufanikiwa kutwaa vijiji 17.

Kwenye mapambano dhidi ya wapiganaji wa kundi la IS wakati wa kuvikomboa vijiji tisa kati ya hivyo, polisi na kikosi cha kupambana na ugaidi wamefanikiwa kuwaua wapiganaji wengi na kuharibu magari 14 yaliyotegwa mabomu.

Hata hivyo taarifa inasema eneo la magharibi litakuwa na changamoto kubwa kutokana na idadi kubwa ya watu wanaofikia laki nane, na kuwa vichochoro vingi vyembamba.

No comments

Powered by Blogger.