Header Ads

Maelfu Wakumbwa Na Hatari Baada Ya Operesheni Ya Kuukomboa Mosul


Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw Farhan Haq amesema maelfu ya familia zinakabiliwa na hatari kubwa baada ya kuanza kwa operesheni ya kutwaa tena udhibiti wa maeneo ya magharibi ya mji wa Mosul, kaskazini mwa Iraq.

Bw Haq amesema kutokana na kuanza kwa opresheni hiyo, mashirika ya kibinadamu yameonya kuwa maelfu ya familia zimekumbwa na matatizo kutokana na kupungua kwa utoaji wa chakula na mafuta, kufungwa kwa masoko na maduka, pamoja na ukosefu wa maji na umeme.

Umoja wa Mataifa umekadiria kuwa watu takriban laki 7.5 hadi laki 8 wanaishi magharibi mwa Mosul.

No comments

Powered by Blogger.