Header Ads

Madhila Ya Arsene Wenger Yamchosha Jens Lehman

Tokeo la picha la Arsene Wenger and Jens Lehman

Aliyekua mlinda mlango mashuhuri wa klabu ya Arsenal Jens Gerhard Lehmann, anaamini klabu hiyo itapata mafanikio ya kutwaa mataji, endapo Arsène Wenger ataondoka.

Lehman ambaye alisajiliwa na Arsene Wenger kwa vipindi viwili tofauti, amesema hayo alipohojiwa na shirika la utangazaji la Uingereza BBC.

Amesema endapo itatokea meneja huyo kutoka Ufaransa anaondoka itakua ni ushindi tosha kwa Arsenal, kutokana na madhila wanayopitia hivi sasa ya kushindwa kujikwamua na vipigo ambavyo vinachangia kushindwa kutwaa mataji.

Lehmann ambaye aliwahi kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani, amekiri kuumizwa na matokeo ya klabu hiyo kwa siku za karibuni, na amesema hadhani kama upande wa wachezaji kuna tatizo zaidi ya mfumo unaotumiwa na Wenger.


Lehmann alikua sehemu ya kikosi cha Arsenal kilichotwaa ubingwa wa England kwa mara ya mwisho msimu wa 2003/04, na alisajiliwa klabuni hapo mwaka 2003 akitokea Borussia Dortmund    na mwaka 2011 alirejea akitokea VfB Stuttgart.

No comments

Powered by Blogger.