Header Ads

Maalim Seif: Sioni Sababu Ya Kuzungumza Na Lipumba

Tokeo la picha la maalim seif sharif hamad

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kuwa madai yaliyotolewa na Profesa Ibrahim Lipumba kuwa hapokei simu zake hayana ukweli wowote.

Ameyasema hayo katika ziara yake ya Bumbwini Unguja, amesema kuwa kumbukmbu zinaonyesha profesa Lipumba alimpigia simu mara moja lakini alikuwa mbali na simu hivyo alilazimika kumpigia lakini hakupokea.

"Ninachoweza kusema profesa Lipumba alinipigia mara moja, na nilipoona simu yake mimi nikampigia lakini hakuipokea, pia siku ya pili nikampigia tena asubuhi lakini hakuipokea,"amesema Maalim.

Maalim Seif amesema kuwa haoni sababu ya kuwa na mazungumzo na profesa Lipumba kwa kile alichodai kuwa si mwanachama tena wa chama hicho.

Aidha, amesema kuwa watafuata taratibu za kisheria  ili kuhakikisha chama hicho kinatatua mgogoro huo na kuwataka wanachama hao kuwa watulivu.

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo amewataka wanachama kushirikiana kwa pamoja na viongozi wakuu wa chama hicho taifa wanaotambuliwa na baraza kuu la uongozi katika kukijenga na kukiimarisha  chama hicho.

No comments

Powered by Blogger.