Header Ads

Libya Yaiomba NATO Kuisaidia Kuendeleza Jeshi Lake

Tokeo la picha la Libya Military Army

Serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya imeomba NATO kuisaidia kuendeleza jeshi lake. 

Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema NATO iko tayari kuisaidia Libya kujenga taasisi imara za ulinzi na usalama, kuimarisha uwezo wake wa kupambana na ugaidi na kudumisha amani. 

Serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya iliundwa kwenye msingi wa makubaliano ya amani yaliyosainiwa kati ya pande zinazozozana, ili kukomesha mgawanyo na kuleta umoja kwa nchi hiyo. 

Mpaka sasa mgawanyo na machafuko bado vinaendelea kutokana na pande tatu kugombea madaraka ya nchi hiyo.

No comments

Powered by Blogger.