Header Ads

Leonardo Bonucci Kukaa Jukwaani

Tokeo la picha la Leonardo Bonucci and Max Allegri

Beki wa kati wa mabingwa wa soka nchini italia Juventus FC Leonardo Bonucci ataukosa mchezo wa mkondo wa kwanza wa 16 bora wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya FC Porto ambao utachezwa baadae mjini Porto nchini Ureno.

Meneja wa Juventus Max Allegri amethibitisha taarifa za mchezaji huyo kukosa mchezo wa leo, alipozungumza na waandishi wa habari katika mkutano maalum uliofanyika mjini Porto.

Allegri alisema sababu kubwa ya beki huyo kukosa mchezo wa leo inatokana na utovu wa nidhamu aliouonyesha mwishoni mwa juma lililopita wakati wa mchezo wa ligi ya Italia dhidi ya Palermo ambao walikubalia kufungwa mabao manne kwa moja.

Bonucci aliliripotiwa kurushina maneno mazito na meneja huyo mara baada ya mchezo dhidi ya Parlemo katika vyumba vya kubadilishia, lakini mpaka sasa sababu ya mkwaruzano huo haijatajwa.

“Kesho (Leo) Bonucci hatocheza na wala hatokua sehemu ya wachezaji wa akiba. Kwangu jambo hilo ni la kawaida, kutokana na kuamini wachezaji wote wa Juventus wana uwezo sawa bila kujali jina la mtu.


Hata hivyo wakati wa mazoezi ya mwisho ya Juventis katika uwanja wa do Dragao hapo jana, Bonucci alijitenga na wenzake huku akiwa anaasikiliza muziki kwa kutumia kifaa vya masikioni (headphones).

No comments

Powered by Blogger.