Header Ads

Leicester City Yaibanjua Liverpool

Tokeo la picha la Leicester City 3-1 liverpool - sky sports
Majogoo wa jiji Liverpool wameshindwa kufua dafu mbele ya mabingwa watetezi wa ligi ya nchini England Leicester City, kwa kukubali kichapo cha mabao matatu kwa moja.
Liverpool wamekubali kipigo hicho wakiwa kwenye uwanja wa King Power, ambapo Leicester City walicheza kwa mara ya kwanza tangu kuondoka kwa Claudio Ranieri, ambaye alitimuliwa klabuni hapo mwishoni mwa juma lililopita.
Mabao ya mabingwa hao watetezi yalifungwa na mshambuliaji Jamie Vardy aliyefunga mawili dakika ya 28 na  60 huku kiungo Danny Drinkwater akifunga dakika ya 39.
Bao la Liverpool lilikwamishwa wavuni na kiungo mshambuliaji Philipe Coutinho dakika ya 68.
Ushindi huo umeisaidia Leicester City kuondokana na janga la kuingia katika shimo la timu zinazoshika mkia kwa sasa kwenye msimamo wa ligi, kwani kabla ya kuapmbana na Liverpool walikua hawatakiwi kupoteza mchezo.

Kwa sasa The Foxes wamechupa hadi katika nafasi ya 15 kwa kufikisha point 24. Liverpool wameendelea kusalia kwenye nafasi ya tano kwa kumiliki point 49.

No comments

Powered by Blogger.