Header Ads

Kesi Ya Rais Wa Korea Kusini Kuuguruma Februari 27

Tokeo la picha la Park Geun-hye

Mahakama ya katiba ya Korea Kusini imetangaza kuwa kesi ya kumwondoa madarakani rais Park Geun-hye wa nchi hiyo itasikilizwa mara ya mwisho tarehe 27 mwezi huu baada ya kuahirishwa kutoka tarehe 24 kama ilivyopangwa. 

Kwa mujibu wa Ikulu ya nchi hiyo, rais Park Geun-hye bado hajaamua kama atafika mahakamani au la kusikiliza kesi yake. Kama kesi hiyo ikipitishwa, rais Park Geun-hye ataondolewa madarakani na Korea Kusini itafanya uchaguzi mkuu ndani ya siku 60 kwa mujibu wa katiba ya nchi.

No comments

Powered by Blogger.