Header Ads

Kenya Yapongeza Juhudi Za China Katika Uhifadhi Wa Wanyamapori


Waziri wa mazingira na maliasili nchini Kenya Judi Wakhungu amepongeza juhudi za China katika kulinda wanyamapori, huku akisema amri ya kupiga marufuku biashara ya pembe za ndovu iliyotolewa na China itatoa mchango mkubwa katika ulinzi wa tembo Afrika Mashariki.

Wakhungu amesema hayo katika maadhimisho ya miaka 60 ya Shirika la Kuhifadhi Wanyamapori la Afrika Mashariki EAWLS. Waziri huyo pia amesema, ushirikiano na China katika kulinda wanyamapori unaendelea hatua kwa hatua.

No comments

Powered by Blogger.