Header Ads

Kenya Yalalamikia Migawanyiko Kwa Misngi Ya Lugha Barani Afrika


Kenya imelalamikia ukosefu wa Umoja barani Afrika na kulaumu migawanyiko kwa misngi ya lugha.

Hii ni baada ya muwaniaji wa uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Amina Mohamed kupoteza kwa Mouso Faki Mahamat kutoka Chad katika uchanguzi uliofanyika siku ya jumatatu tarehe 30 mjini Addis Ababa.

Aden Duale kiongozi wa wengi kwenye bunge la Kenya na mbuge wa Garissa Mjini, amesema kwamba serikali iliwekeza sana katika kampeni ya Bi Amina Mohamed, lakini kuna mambo kadhaa ambayo yalizingatiwa katika uchanguzi huo.

"Kwanza ni miungano ya kikanda, ECOWAS, SADC, Jumuiya ya Afrika Mashariki na sehemu za kaskazini mwa Afrika hizo ndizo ziliamua jinsi uchanguzi ungefanyika na jambo la pili ni kuingia kwa Morroco tena katika Umoja wa Afrika" Anasema Duale.

Amesema Kenya ilikuwa iashiriki katika uchanguzi huo kwa ajenda ya mageuzi lakini hata hivyo anaona kwamba kama nchi hawajapoteza bali wamefaidi amesema.

"Kama nchi tumefaidi hatUjapoteza tulienda miji mingi, tuna marafiki wengi, tuna nchi 26 ambazo ziko kwa upande wetu sasa, kwa hivyo hiyo miezi wanne ya kampeni imetulea faida nyingi na pia tumejua ni nani ni rafiki yetu na nina si rafiki yetu"

Amina Mohamed ambaye ni waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi hilo la ushaguzi analalamika kwamba Bara la Afrika limegawanyika katika mistari ya lugha.

"Ni huzuni bara la Afrika limegawanyishwa na lugha na ilhali hizo lugha si zetu na wenye hizo lugha awapigani miongoni mwao, na nadhani hiyo ndio jambo moja linalopaswa kuangaliwa kwa sababu kama halitaangaliwa basi litaendelea kugawanyisha bara la Afrika"

Awali wadhifa huo ulishikiliwa na bibi Dlamini Zuma wa Afrika Kusini na naibu wake Erastus Mwencha kutoka Kenya.

No comments

Powered by Blogger.