Header Ads

Kenya Kukusanya Fedha Kutoka Kwa Wahisani Na Sekta Binafsi Kukabiliana Na Ukame

Tokeo la picha la Joseph Kinyua

Kenya ina lengo la kukusanya fedha kutoka kwa wadau mbalimbali na mashirika ya Kenya kuunga mkono utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa watu wapatao milioni 3 walioathiriwa na ukame.

Mkuu wa idara ya utumishi ya Kenya  Joseph Kinyua amesema serikali inakamilisha majadiliano na wadau wa maendeleo, mashirika ya misaada na sekta binafsi kutafuta njia kuupatia fedha mfuko wa kupambana na ukame. 

Amesema makadirio yaliyofanywa yanaonesha kuwa misukosuko ya kibinadamu inayohusiana na ukame imekuwa mikubwa, na inahitaji mashirika ya kimataifa na binafsi kuchangia kwenye mfuko chakula cha msaada kwa ajili ya kaunti zilizoathiriwa.

Bw Kinyua amesema Marekani, China na Umoja wa Ulaya wameonyesha utayari wa kuchangia kwenye mfuko huo.

No comments

Powered by Blogger.