Header Ads

Kanuni Zaipa Meno FC Barcelona

Tokeo la picha la Aleix Vidal injury

Mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona wanaruhusiwa kufanya usajili wa kuziba nafasi ya beki wa pembeni Aleix Vidal ambaye mwishoni mwa juma lililopita alipata majeraja ya mguu.

FC Barcelona wanaruhusiswa kufanya hivyo kwa mujibu wa kanuni za ligi ya nchini Hispania (La Liga), ambazo zinatoa nafasi kwa klabu yoyote kusajili endapo mchezaji atapatwa na majeraha makubwa ambayo yatamuweka nje kwa kipindi kirefu.

Vidal alipatwa na majeraha ya kifundo cha mguu, wakati wa mchezo wa ligi wa mwishoni mwa juma lililopita, ambapo FC Barcelona walichomoza na ushindi wa mabao sita kwa sifuri dhidi ya Alaves.

Kutokana na tukio hilo Luis Enrique ambaye anakabiliwa na ukata wa mabeki wa kulia kwa sasa, atazimika kumtumia Sergi Roberto ama Javier Mascherano katika nafasi hiyo wakati akisubiri kufanya maamuzi ya kusajili.

Hata hivyo kanuni hiyo haiipi nafasi FC Barcelona kumtumia mchezo watakaemsajili kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Taarifa za awali zinadai kwamba FC Barcelona huenda wakamsajili Nili Perdomo.

No comments

Powered by Blogger.