Header Ads

Jose Mourinho Aanza Kujihami

Tokeo la picha la FA Cup Quater final 2017

Meneja wa Man Utd Jose Mourinho ameanza kujihami, kufuatia ratiba ya robo fainali ya kombe la FA ambayo inaonyesha atapambana na waajiri wake wa zamani Chelsea FC.

Mourinho alikiongoza kikosi chake kupata ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Blackburbn Rovers katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya kombe la FA hapo jana, amesema Chelsea wana nafasi kubwa ya kufanya vyema katika mchezo wa robo fainali kutokana na kuwa na fikra za ubingwa.

Amesema kitendo cha kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi ya nchini England kwa tofauti ya point tisa, kitawasaidia Chelsea kujiamini katika mpambano wao dhidi ya Man Utd, hivyo hana budi kusaka mbinu za kupambana kisawa sawa.

Ratiba ya robo fainali ya kombe la FA, ilitolewa dakika chache baada ya kipyenga cha mwisho cha mchezo wa Blackburn Rovers dhidi ya Man utd kupulizwa.

Chelsea walifanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya kombe la FA, kwa kuifunga Wolves mabao mawili kwa sifuri siku ya jumamosi.

Ratiba kamili ya robo fainali ya kombe la FA.

Chelsea v Manchester United
Middlesbrough v Huddersfield Town/Manchester City
Sutton United/Arsenal v Lincoln
Tottenham Hotspur v Millwall


Michezo ya robo fainali ya kombe la FA imepangwa kuchezwa Machi 11 na 12.

No comments

Powered by Blogger.