Header Ads

IGAD Kufanya Mkutano Maalumu Juu Ya Wakimbizi Wa Somalia

Tokeo la picha la IGAD

Jumuiya ya Maendeleo ya serikali ya nchi za Afrika Mashariki IGAD imetangaza kufanya mkutano maalumu mjini Nairobi Machi 25, ili kusaidia kutafuta suluhu ya kudumu kwa wakimbizi wa Somalia.

Jumuiya hiyo inayoundwa na Kenya, Uganda, Somalia, Djibouti, Sudan, Ethiopia, Eritrea na Sudan Kusini imesema mkutano huo utahimiza maendeleo yaliyopatikana karibuni katika ngazi ya taifa, kikanda na dunia ili kutoa hifadhi na ulinzi kwa maelfu ya wakimbizi wa Somalia ambao bado wana mahitaji. 

Mkutano huo maalumu uliamuliwa kufanyika katika mkutano wa kawaida wa IGAD uliokutanisha wakuu wa nchi na serikali ambao ulifanyika Septemba 13 2016, Mogadishu Somalia.

Zaidi ya Wasomali milioni 2 wamekimbia makazi yao kutokana na mgogoro mkubwa ambao sasa umeingia katika muongo wa tatu.

No comments

Powered by Blogger.