Header Ads

Hugo Broos Ajaribu Kuikimbia Cameroon

Tokeo la picha la hugo broos
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Cameroon Hugo Broos, huenda akaachana na timu hiyo kufuatia kutuma maombi kwenye chama cha soka Afrika kusini (SAFA).
Broos, alichukua hatua hiyo siku 11 zilizopita, na jina lake limeonekana kwenye orodha ya wanaowania kiti cha ukuu wa benchi la ufundi la Bafana Bafana, ambacho kipo wazi tangu mwishoni mwa mwaka jana, baada ya kutimuliwa kwa Ephraim 'Shakes' Mashaba.
Katika kuiwania nafasi hiyo, kocha huyo kutoka nchini Ubelgiji, atapambana na wataliano Roberto Mancini na Giovanni Trapattoni, Wajerumani Lothas Matthaus na Bernd Schuster.
Hassan Shehata, ambaye aliiwezesha Misri kutwaa ubingwa wa Afrika mara tatu mfululizo (2006,2018,2010) naye ni miongoni mwa walioomba nafasi ya kutaka kuwa kocha mkuu wa Bafana Bafana pamoja na gwiji wa soka kutoka Nigeria Samson Siasia.
Chama cha soka Afrika kusini (SAFA), kimetangaza kamti maalum ambayo itasimamia zoezi la mchujo wa makocha walioomba nafasi ya kutaka kuifundisha Bafana Bafana, kabla ya kuanza mchakato wa mwisho wa kuwafanyia usaili wachache watakaobaki.

Miongoni mwa wanaounda kamati hio ni wachezaji wa zamani wa Bafana Bafana Lucas Radebe na Benni McCarthy.

No comments

Powered by Blogger.