Header Ads

Harry Redknapp Awapa Ushauri Wa Bure Liverpool

Tokeo la picha la Harry Redknapp and Joe Hart - sky sports

Aliyekua meneja wa klabu ya Tottenham Hotspur Harry Redknapp anaamini mlinda mlango wa Manchester City anaecheza kwa mkopo nchini Italia Joe Hart, ni suluhisho tosha la ulinzi wa lango la Liverpool.

Hart ambaye alilazimika kujiunga na klabu ya Torino kwa mkopo, baada ya kushindwa kumshawishi meneja wa sasa wa Man City Pep Guardiola, amekua anatajwa katika mpango wa kusajiliwana klabu ya Arsenal itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Redknapp amesema mpango huo wa Arsenal sio sahihi kutokana na tatizo la klabu hiyo kutokua sehemu ya ulinzi wa lango, na kwa upande wake anaamini Hart atakuwa suluhisho kwa Liverpool kama watajitokeza na kuingia katika vita ya kumuwania.

Amesema Liverpool imekua na msimu mzuri, lakini wanakwamishwa na tatizo la ulinzi wa lango ambao upo mikononi mwa Simon Mignolet akisaidiana na Loris Karius.

Babu huyo ameongeza kuwa, wawili hao wameshindwa kuitendea haki klabu hiyo kongwe ya Anfield na kujikuta wakiirudishwa nyuma kwenye harakati za kuwania ubingwa msimu huu.

Tokeo la picha la Harry Redknapp and Joe Hart - sky sportsHarry Redknapp

"Ninaamini kama Liverpool wangekua na mlinda mlango kama Hart, wasingekua walipo sasa, wampoteza muelekeo kabisa wa ushindani wa ubingwa msimu huu," Redknapp aliiambia Betsafe.

"Hart ana sifa za kipekee na kama kweli Man City watakuwa tayari kumuweka sokoni, ninaishauri Liverpool isilaze damu, wahakikishe wanamsajili kwa gharama yoyote."

"Kuhusu Arsenal kuhusishwa na usajili wa Hart mwishoni mwa msimu huu, siamini kama klabu hii ina tatizo la mlinda mlango, na kama itatokea wanamsajili itakua ni kazi bure."


Harry Redknapp kwa mara ya mwisho alionekana katika benchi la ufundi akiwa kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya Jordan, lakini hakudumu kwenye timu hiyo.

No comments

Powered by Blogger.