Header Ads

Guedes Ataja Sababu Za Kuimwaga Man Utd


Mshambuliaji mpya wa klabu bingwa nchini Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG) Gonçalo Manuel Ganchinho Guedes, amefunguka kuhusu maamuzi ya kuitema Man Utd wakati wa usajili wa dirisha dogo.

Mshambuliaji huyo alikua akiitumikia klabu ya Benfica ya nchini kwao Ureno, aliwekwa njia panda kwa kutakiwa kufanya maamuzi ya kujiunga na PSG au Man Utd, baada ya uliokua uongozi wake kupokea ofa kutoka Ufaransa na England.

Guedes mwenye umri wa miaka 20, ametoa ufafanuzi wa kuikataa Man Utd na kuichagua PSG alipozungumza na RMC: "Siku zote nilikua ninaota kuwa sehemu ya kikosi cha PSG.

"Ninafahamu vizuri kuhusu soka la England na Ufaransa, kuna tofauti kubwa linapokuja suala la ushindani, lakini kwa umri wangu ninaamini ilikua ni mapema mno kwenda Old Trafford na ndio maana nikaamua kuichagua PSG. Man utd kuna mazingira mazuri ya kucheza soka, lakini nimeona bado wakati wake haujafika.”


"Kwa hapa jijini Paris ninajihisi nipo nyumbani, tofauti ningechagua kwenda England kwa umri wangu."

No comments

Powered by Blogger.