Header Ads

Giampiero Ventura Atia Shaka Suala La Federico Fazio

Tokeo la picha la Federico Fazio - Sky sportsFederico Fazio

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Italia Giampiero Ventura amempotezea beki wa klabu ya AS Roma  Federico Fazio ambaye ameonyesha kuwa tayari kuitumikia The Azzurri.

Beki huyo mzaliwa wa Argentina, aliweka wazi dhamira yake juma lililopita ya kutaka kuwa sehemu ya kikosi cha Italia, kutokana na kuona umuhimu wa kulitumikia taifa hilo ambalo limemkuza kisoka.

“Kilamtu anataka kuwa mtaliano, lakini jambo la msingi tunataka kuona umuhimu wa mtu na uwajibikaji wake ili tuweze kumuita katika kikosi cha timu yetu ya taifa na sio vinginevyo!" Ventura aliwaambia waandishi wa habari.

“Kwa umakini mkubwa nitalifuatilia jambo hilo ili nijiridhishe kama kweli Fazio ana nia ya kuwa sehemu ya kikosi chetu, Pia itanilazimu kuangalia upande wa kanuni na taratibu za FIFA ili kuona kama tuna uwezeo wa kumtumia katika taifa letu na sio kukurupuka. Fazio ni mchezaji muhimu akiwa na AS Roma, na ninaomba nieleweke kuwa sio ninamkataa lakini taratibu lazima zifuatwe. Alisema kocha huyo.

No comments

Powered by Blogger.