Header Ads

Gerard Pique Azinguana Na Luis Suarez, Jordi Alba

Tokeo la picha la Gerard Pique, Luis Suarez and Jordi Alba

Beki wa FC Barcelona Gerard Pique ameripotiwa kushikana mashati na mshambuliaji Luis Suarez, baada ya kuchukizwa na matokeo ya kufungwa mabao manne kwa sifuri dhidi ya PSG usiku wa kuamkia jana.

Jarida la Don Balon limeripoti kuwa, Pique alifikia hatua hiyo baada ya kutopendezwa na juhudi za Suarez katika mchezo dhidi PSG, huku akiamini mshambuliaji huyo kutoka nchini Uruguay alikua kikwazo cha kushindwa kuikwamua Barcelona katika aibu iliyowakuta jijini Paris.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 30 pia alimjumuisha Jordi Alba kwenye ugmvi huo, kufuatia beki huyo wa pembeni kumtetea Suarez.


Hata hivyo wachezaji wengine wa Barcelona waliwasihi kuacha mvurugano huo, na baadae hali ilirejea kuwa shwari walipokua katika vyumba vya kubadilishia.

No comments

Powered by Blogger.