Header Ads

Florentino Perez Kuichokonoa FC Barcelona

Picha inayohusiana

Ni kama hadithi za abunuwasi, lakini ukweli ni kwamba rais wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid Florentino Perez ameanza uchokonozi wa kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Brazil na FC Barcelona Neymar da Silva Santos JĂșnior.

Jarida la Don Balon limefanya uchunguzi wa kina na kubaini ukweli wa jambo hilo, ambalo linapewa msukumo na rafiki wa karibu wa kiongozi huyo, ambaye hana tatizo linapokuja suala la matumizi ya fedha kwa ajili ya usajili wa wachezaji wenye thamani kubwa duniani.

Jarida hilo limeeleza kuwa, Perez ametenga kiasi cha Euro milioni 200 kwa ajili ya kumng’oa Neymar Camp Nou, na anaamini jambo hilo linawezekana licha kuwepo kwa uhasimu baina ya Real Madrid na FC Barcelona.

Perez aliwahi kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Ureno Luis Figo akitokea FC Barcelona mwaka 2000 kwa  dola za kimarekani milioni 60.1, hali ambayo ilizua tafrani miongoni mwa mashabiki wa mabingwa hao wa sasa nchini Hispania.


Hii itakua mara ya pili kwa Neymar kuhusishwa na mpango wa kusajiliwa akiwa FC Barcelona, baada ya rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi kujaribu kufanya hivyo kwa kitita cha Pauni milioni 170 mwishoni mwa msimu wa 2015/16, lakini ilishindikana.

No comments

Powered by Blogger.