Header Ads

FC Bayern Munich Yaiadhibu Tena Arsenal


Mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich wameutumia vyema uwanja wao wa nyumbani Allianz Arena kwa kuichapa Arsenal mabao matano kwa moja, katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya usiku wa kuamkia leo.

FC Bayern Munich ambao ni wababe wa Arsenal kwenye michuano hiyo, walipata mabao yao kupitia kwa Arjen Robben, Robert Lewandowski, Thomas Muller pamoja na Thiago Alcantara aliyefunga mabao mawili.

Bao la kufutia machozi kwa upande wa Arsenal lilifungwa na mshambuliaji kutoka nchini Chile Alexis Sanchez.

Kipigo hicho kwa Arsenal ni kama fedheha kwa meneja wao Arsene Wenger, ambaye kwa siku za karibuni amepoteza michezo muhimu ya ligi ya nchini England na huo wa ligi ya mabingwa.


Kwa ushindi wa FC Bayern Munich, Arsenal wamejiweka kwenye mazingira magumu ya kusonga mbele katika michuano hiyo, kutokana na hitaji la mabao manne kwa sifuri watakapowakaribisha The Bavarians jijini London, majuma mawili yajayo.

No comments

Powered by Blogger.