Header Ads

FC Barcelona Wapinga Adhabu Ya Suarez, Busquets


Klabu ya Barcelona imewasilisha rufaa ya kupinga adhabu ya kadi nyekundi iliyomshukia mshambuliaji Luis Suarez wakati wa mchezo mkondo wa pili wa nusu fainali ya kombe la Mfalme,  dhidi ya Atletico Madrid uliochezwa usiku wa kuamkia jana.

FC Barcelona ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo, wamethibitisha kukata rufaa ya kupinga adhabu hiyo, kwa kuuarifu umma wa mashabiki kupitia tovuti ya www.fcbarcelona.com.

Taarifa hiyo pia imesisitiza kupingwa kwa adhabu ya kadi ya njano ya aliyoonyeshwa Sergio Busquets ambayo inamnyima nafasi ya kuchezo mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la Mfalme ambapo watapambana Alaves mwezi Mei.

Hata hivyo taarifa hizo zimedai kuwa, klabu hiyo haijapinga adhabu ya kadi nyekudu aliyoonyeshwa beki Sergi Roberto kwa madai haikugubikwa na utata wa kimaamuzi.

Mwamuzi Jesus Gil Manzano amesema alifanya maamuzi ya kumuadhibu Suarez katika dakika ya 90, kufuatia kosa la kumsukuma kwa mkono mchezaji wa Atletico Madrid Koke, alipokua kwenye harakati za kuwania mpira huku adhabu ya Busquets ilitokana na kuupiga mpira kwa makusudi ili-hali filimbi ikiwa imeshapulizwa.

Wakati huo huo Barca wamethibitisha kuumia kwa kiungo mkabaji Javier Mascherano na atakosa mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Alaves pamoja na ule wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Paris St Germain.


Mascherano alipatwa na maumivu ya nyama za paja akiwa katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya kombe la mfalme dhidi ya Atletico Madrid.

No comments

Powered by Blogger.