Header Ads

FC Barcelona Wamgeukia Laurent Blanc

Tokeo la picha la Laurent Blanc and Luis Enrique

Aliyekua meneja wa mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG Laurent Blanc ameripotiwa kuwa katika mazungumzo na viongozi wa FC Barcelona.

Blanc ambaye aliwahi kuitumikia Barca kama mchezaji kuanzia mwaka 1996 hadi 1997, anatajwa kuwa katika mazungumzo na uongozi wa mabingwa hao wa Hispania kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Luis Enrique.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini Ufaransa vimeripoti uwepo wa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, na kuna matarajio makubwa zikafikia muafaka wakati wowote kuanzia sasa.

Blanc kwa sasa hana kazi, baada ya kuondoka PSG mwishoni mwa msimu uliopita.


Luis Enrique anatarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu, kutokana na kasi yake ya ukufunzi kushindwa kwenda sambamba na matarajio ya viongozi wa FC Barcelona, kutokana na kikosi chake kukosa ushindani kama ilivyokua misimu miwili iliyopita alipoanza kazi.

No comments

Powered by Blogger.