Header Ads

FAO Yasisitiza Kuendelea Kuunga Mkono Sekta Ya Mifugo Ya Afrika

Tokeo la picha la Patrick Kormawa - FAOPatrick Kormawa

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesisitiza kuwa litaendelea kuunga mkono sekta ya mifugo barani Afrika.

Kwenye kongamano lililozindua mradi unaoitwa ufugaji endelevu wa Afrika 2050 (ASL 2050), mratibu wa FAO kanda ya Afrika Mashariki  Patrick Kormawa amesema ufugaji ambao ni moja ya sekta za kilimo zinazokua kwa kasi barani Afrika, ni sehemu muhimu ya mradi wa shirika hilo barani humo.

Kwa kushirikiana na Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani USAID na nchi sita za Afrika, FAO imezindua mradi wa ASL2050 ili kutimiza ufugaji endelevu barani Afrika.

Kwa mujibu wa data zilizotolewa na shirika hilo, ifikapo mwaka 2050 soko la nyama linatarajiwa kufikia tani milioni 34.8 na soko la maziwa kufikia tani milioni 82.6, ambalo ni ongezeko la asilimia 145 na 155 mtawalia ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2005 hadi 2007.

No comments

Powered by Blogger.