Header Ads

El-Hadj Diouf Awashukia Waliogoma

Gwiji wa soka nchini Senegal, El-Hadj Diouf amesema wachezaji wanane wa Cameroon waliokataa wito wa kuichezea timu yao ya taifa katika fainali za Afrika, watajutia uamuzi huo maisha yao yote.
Nyota kadhaa wa Cameroon akiwemo Joe Matip anayekipiga Liverpool, Eric Choupo-Moting na Allan Nyom walikataa kuitumikia nchi yao kwa madai binafsi haswa suala la kuchelewa kwa posho zao.
Diouf amesema haelewi watu wanaoikataa nchi yao kwa kisingizo cha pesa, jambo ambalo amedai linadhihirisha udhaifu wa uzalendo walionao.

Diouf amesema siku zote ni ngumu kuwa muafrika kwani hata kama ukiwa kocha mzuri namna gani lakini haitowezekana kuwa meneja wa klabu kubwa kama Barcelona, Paris Saint-Germain, Liverpool au Manchester United.

No comments

Powered by Blogger.