Header Ads

Dimitri Payet, Memphis Depay Wazisalim Nyavu Ufaransa


Tokeo la picha la Dimitri Payet and Memphis Depay
Dimitri Payet 

Tokeo la picha la Dimitri Payet and Memphis Depay
Memphis Depay

Wachezaji Dimitri Payet na Memphis Depay wamefunga mabao kwa mara ya kwanza, tangu walipojiunga na klabu za nchini Ufaransa wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi uliopita.

Wawili hao walifunga mabao katika michezo ya ligi ya nchini Ufaransa iliyochezwa usiku wa kuamkia hii leo, ambapo Payet alifunga moja ya mabao mawili yaliyoipa ushindi Olympic Marseille mbele ya Guingamp.

Kwa upande wa Memphis Depay alifunga bao lake katika mchezo dhidi ya Nancy ambao wamekubali kupoteza kwa kupokea kichapo cha mabao manne kwa sifuri dhidi ya Olympic Lyon.

Payet alifunga bao lake kwa njia ya adhabu ndogo (free-kick) huku Depay akifunga kwa njia ya mkwaju wa penati.

Payet alijiunga na Olympic Marseille akitokea West Ham Utd, baada ya kuweka shinikizo la kutaka kuachana na wagonga nyundo hao kwa kipindi cha zaidi ya majuma mawili.

Depay alijiunga na Olympic Lyon akitokea Man Utd, baada ya mambo kumuendea kombo kwa kushindwa kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Jose Mourinho.

Matokeo ya michezo mingine ya ligi ya nchini Ufaransa iliyochezwa usiku wa kuamkia hii leo.

Angers 0 – 0 Rennes
Lorient 1 – 1 Toulouse
Metz 2 – 1 Dijon

Nice 1 – 0 Saint-Etienne

No comments

Powered by Blogger.